Maafa kanisani Kilifi

Familia moja eneo la Mbaoni eneo Bunge la Magarini kaunti ya Kilifi inaomboleza baada ya kuwapoteza watoto wao wawili baada ya jengo la kanisa kuporomoko.

Akizungumza kwa njia ya simu na PwaniFM mmoja wa familia hiyo Vincent Tsofa Kaingu amesema kisa hicho kilitokea siku ya Jumapili waumini walipokuwa wanaendeleza ibada katika kanisa la Imani sehemu hiyo kabla ya tukio hilo kutokea.

Kaingu amesema baadhi ya waumini walipata majeraha mabaya ambapo wengine wanaendelea kupokea matibabu hospitalini na wengine walitibiwa na kuruhusiwa kwenda nyumbani.

Hata hivyo miili ya wawili hao imehifadhiwa katika hifadhi ya maiti katika hospitali ya kaunti ndogo ya Malindi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *