Lengo Ni Kuchezea Harambee Stars Wasema Wachezaji wa Young Strikers

Soka ni mchezo ambao unashabikiwa na wengi hapa nchi na ulimwengu kwa ujumla na hilo si tofauti kwa vijana Brian Rimba na Dylan Tsui Denje ambao wamejitokeza kutambulisha kipaji chao.

Brian Fondo mwenye umri wa miaka 20 anayecheza katika safu ya mashambulizi kwenye timu ya Young Strikers ya kijijini Somali eneo bunge la Rabai ni kijana ambaye ameweka wazi kuwa anatafuta mafanikio katika mchezo wa soka na lengo lake kubwa ni kuchezea kilabu ya Ulinzi stars humu nchini pamoja na timu ya taifa Harambee Stars

Fondo anaamini weledi wake katika usakataji soka utafanikisha azma yake ya kuchezea timu ya taifa.

“Lengo langu ni kuhakikisha nafaidika na kipaji changu na kufanikisha ndoto zangu za kucheza barani ulaya ambapo namatamanio ya kuchezea timu ya Chelsea”. Amesema Fondo.

Pia ameweka wazi kuwa anapenda usakataji soka wa mchezaji wa Juventus na Ureno Cristiano Ronaldo na hapa nchini anapenda uchezaji wake Michael Olunga.

Kwa upande wake mshambulizi mwenza wa timu hio Dylan Tsui Denje mwenye umri wa miaka 18 naye hajasazwa nyuma kwani ni mmoja wa washambulizi hatari wanaoinukia kisoka kwenye eneo hilo la Somali na mara nyingi amekua akisema kuwa angependa kuwa kama Dennis Oliech na kuiwakilisha Kenya kwenye michuano ya kimataifa.

Denje ambaye ni shabiki mkubwa wa timu ya Arsenal anamuenzi sana mshambulizi nguli wa timu hio Pierre Emmerick Aubameyang na anasema lengo lake kuu ni kuendeleza kipaji chake na kuhakikisha anafikia upeo wa juu.

Akizungumza na meza yetu ya michezo Denje ameweka wazi kuwa soka imeweza kumuweka kando na mambo maovu yakiwemo utumiaji wa dawa za kulevya na anawasihi vijana wenzake kuendeleza vipaji vyao na kujiepusha na dawa za kulevya. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *