Kilifi: Wadau wataka serikali kupiga marufuku ukataji wa mikoko

Wadau wa kuhifadhi misitu ya mikoko katika kaunti ya Kilifi sasa wanavitaka vyama vya kisiasa kuwekeza zaidi katika uhifadhi wa mazingira.

Uharibifu wa mazingira ya pwani haswa ukataji wa mikoko uliilazimu serikali kupiga marufuku ukataji mikoko katika kaunti za Kilifi, Kwale na Mombasa.

Hata hivyo marufuku hiyo iliondolewa katika kaunti ya Lamu kwa sababu wakaazi walitii masharti ya utunzaji wa mazingira.Wanamazingira hao walipanda miche 1,500 ya mikoko katika eneo la Mida.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *