Kanye akojolea Tuzo ya Grammy, huku akianzisha vita dhidi ya label za muziki

Kanye akojolea Tuzo ya Grammy, huku akianzisha vita dhidi ya label za muziki

Rapper Kanye West ameachia kipande cha video cha kushangaza kwenye ukurasa wake wa Twitter kilicho mwonyesha akienda haja ndogo juu ya tuzo ya Grammy.

Kanye ameshinda Tuzo 21 za grammy katika kipindi cha muda wa miaka 20

Rapper huyo pia ameanzisha vita vikali kwenye mtandao wa twitter akilenga kupata umiliki wa kazi zake za usaani toka katika kapuni ya Universal Music Group na Sony.

 Kupitia Tweets aliachia kwenye mtandao wa Twitter Kanye amedai kuwa Labels za Miziki kote duniani zimetayarisha kandarasi na mikataba yao kuwanufaisha wao wenyewe bila ya kumnufaisha msaani.

Kanye pia amechapisha nakala za mikatba yote ya kimziki aliowahi kusani huku akiwataka mawakili kuyasoma.

Aidha amedai kuwa Universal Music wameshindwa kumweleza bei ya kumiliki Masters za kazi zake za kisaani kwasababu anahela na uwezo wa kuzinunua.

Rapper huyo mwenye ushawishi mkubwa kwenye mtandao wa Twitter ameongeza kuwa hakuna msaani anayetengeza mamilioni ya fedha kwenye usaani kutoka na mikataba ya kikandamizaji.

Vile vile amesema kuwa hataachia mziki mpya hadi pale atakapo miliki masters za kazi zake za awali, inasemekanakuwa kuwa masters za kazi za awali za Kanye huenda ikafikia dolla millioni 300

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *