Kagwe, komesha safari za kwenda mashambani

Waziri wa Afya Mutahi Kagwe, amekariri wito wake kwa Wakeenya kujiepusha na safari zizizo muhimu za kwenda maeneo ya mashambani ili kuzuia kusamabaa kwa maradhi ya COVID-19.

Kagwe alisema ni jambo la kusikitisha kuwa watu 48 wa familia moja wamepatikana kuwa na virusi vya Corona baada ya mmoja wao anayeishi jijini Nairobi kuwatembelea.

Kagwe alionya kuwa watu wazee ambao wengi wao wanaishi mashambani wamo katika hatari kubwa ya kuathirika na maradhi ya COVID-19, na hivyo basi kuna haja ya kuwalinda kwa kujiepusha na safari ambazo hazifai.

Alisema maradhi hayo yamesambaa miongoni mwa watu wa vizazi vitatu kwenye familia moja katika kaunti ya Migori.

Kagwe kadhalika alitoa wito kwa kila mtu kuwajibika ili kuzuia kusambaa kwa maradhi ya COVID-19.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *