Hatma ya maseneta watano wa Jubilee kujulikana wiki ijayo

Hatma ya maseneta watano wa chama Jubilee ambao walisusia kuhudhuria mkutano wa chama ulioitishwa na kinara wa chama hicho Rais Uhuru Kenyatta mwezi Mei itajulikana wiki ijayo.

Halmashauri Kuu ya Kitaifa ya chama hicho inatazamiwa kupitisha maazimio ya kamati ya nidhamu ambayo ilikaa chini kuchunguza nyendo zao.

Kamati ya Nidhamu ya Chama cha Jubilee iliyoongozwa na Lumatete Muchai ilimaliza mahojiano yake juu ya uwasilishaji wa mawasilisho na maseneta hao miezi miwili iliyopita na tangu wakati huo kumekuwa na kimya juu ya suala hilo.

Aidha watano hao wanaolengwa ni maseneta wateule Millicent Omanga, Mary Seneta Yiane, Falhada Dekow Iman, Naomi Jillo Waqo na Alice Milgo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *