Gavana Ali Korane wa Garisa aachiliwa kwa dhamana

Gavana wa garisa Ali Korane ameachiliwa kwa dhamana ya shilingi milioni 3.2huku mahakama ikimuzuia kuingia ofisini pamoja na washukiwa wenzake.

Washukiwa wenzake wameachiliwa kwa dhamana ya shilingi milioni1.2 kila mmoja.Wakati huo huo mahakama imeamrisha washukiwa waache passport zao mahakamani na waliitafiane na mashahidi.

Gavana Korane anakabiliwa na tuhuma za ufujaji wa zaidi ya shilingi milioni 233 zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya maendeleo.

Wakati wa kusikizwa kwa kesi yake mawakili wa gavana korane wakiongzwa na Abdinassir Abdillahi wamesema mteja wao hajahusika kivyovyo na wizi wa mali za umma.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *