Diamond League yafutiliwa mbali kutokana na virusi vya Corona.

Mashindano ya riadha ya Diamond league ambayo yalikuwa yameahirishwa hadi tarehe 12 mwezi Septemba mjini Gateshead Uingereza yamefutiliwa mbali kutokana na janga la virusi vya Corona.

Awali, mbio hizo zilikuwa zimeratibiwa kuandaliwa tarehe 16 mwezi ujao. Waandalizi wamesema kuwa kanuni zilizowekwa na serikali za kukabliana na kusambaa kwa virusi vya Corona vilitatiza ukarabati wa uwanja wa kimataifa wa Gateshead ambao ungeandaa mashindano hayo.

Kalenda ya mbio za riadha mwaka huu imetatizwa mno na janga la virusi vya Corona na limesababisha kuahirishwa kwa michezo ya Olimpiki jijini Tokyo hadi mwaka ujao.

Mashindano ya riadha ya Diamond League jijini London, Rabat, Zurich, Paris na Eugene pia yamefutiliwa mbali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *