Chidzuga anamtaka kamishna wa Kwale kuchapisha orodha ya wazi orodha ya wanonufaika na mpango wa serikali wakati wa Covid-19

Mkurugenzi katika Bodi ya Unyunyiziaji Nchini Zainabu Chidzuga anamtaka Kamishna wa Kwale Karuku Ngumo kuweka wazi orodha ya majina ya watu walioko katika mpango wa serikali wakupokea shilingi 2,000 kila mwezi baada ya kuathirika na msambao wa Corona.

Akizungumza mjini Kwale Chidzuga ametilia shaka endapo wakaazi waliorabitiwa kupokea jumla ya shilingi 2,000 kusini mwa pwani wamefaidika tangu mpango huo kubuniwa.

Kadhalka amedokeza kwamba endapo hakutakuwa na uwazi na usawa katika mpango huo basi huenda ukahujumu juhudi za serikali.

Moses Odhiambo ni mmoja wa wakaazi waliorodheshwa katika mpango huo miezi mitatu iliyopita ila hadi sasa hajapokea chochote.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *