Chamuko jipya la Covid-19 laripotiwa Ulaya

Chamuko jipya la virusi vya corona barani Ulaya limefikisha milioni tatu visa vya maambukizi ya virusi hivyo barani humo.

Bara hilo lingali na idadi kubwa zaidi ya vifo vilivyotokana na ugonjwa wa Covid 19 huku likinakili vifo vya watu 206,633 kati ya vifo 627,307 vilivyonakiliwa kote duniani.

Mpango wa yuro bilioni 750 wa ufufuzi wa uchumi kufuatia janga la corona uliafikiwa wakati wa kongamano la muungano wa Ulaya wiki hii.

Hata hivyo umoja wa mataifa umetoa wito wa kutolewa kwa mapato ya kimsingi kwa mataifa maskini zaidi duniani ili kupunguza maambukizi ya ugonjwa wa COVID-19.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *