Chama Cha KANU Chaimarishwa Mombasa

Uongozi wa kamati ya chama cha KANU kaunti ya Mombasa wameanza mchakato wa kukiimarisha chama hicho kwenye harakati za kujiandaa katika uchaguzi mkuu mwaka wa 2022.

Wakiongozwa na mwenyekiti wao Bi. Rukia , wameeleza kuwa sasa chama cha KANU kitaanza kuingia mashinani na kuwajuza wakaazi kuhusu muamko wao mpya kwa kile anachokitaja kuwa awali walikuwa hawajajitambulisha vya kutosha.

Kadhalika Rashid ameeleza kuwa miongoni mwa changamoto ambazo chama cha KANU wamegundua mashinani na wanatarajia kujadiliana na serikali ya kaunti ni ukosefu wa umeme na maji miongoni mwa maswala mengine tata.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *