Cardi adai Talaka kwa Offset

Rappa  wa marekani Belcalis Marlenis Almanzar aka Card B amewasilisha kesi katika mahakama moja ya mjini Atalanta kutaka talaka toka kwa mume wake wa miaka mitatu rappa Offset.

Cardi B na Offset walifunga ndoa mwaka wa 2017 na wana mtoto wa mika miwili anaye fahamikakama Culture.

Kwa mujibu wa stakabadhi zilizo mahakamni mjini Georgia Cardi anataka apatie jukumu la kumulea Culture huku Offset akigharamiamahitaji yake yote.

Tofauti kati yao ilitokea mara ya kwanza mwaka wa 2018 baada ya Cardi kuachia ujumbe kwenye ukurasa wake wa Twitter ulioashiria kuwa walikuwa wametengana kabla ya kumaliza tofauti hizo.

 Kesi yao itasikizwa mapema mwezi November mjini Georgia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *