Buhari wa Nigeria ametangaza safari yake ya kwanza baada ya miezi kadhaa

Rais Muhammadu Buhari wa Nigeria ametangaza safari yake ya kwanza baada ya miezi kadhaa huku afisi yake ikithibitisha kuwa atakuwa anaungana na marais wengine wanne katika mazungumzo ya kujaribu kuleta amani nchini Mali.

Wapatanishi wa eneo hilo wameimarisha juhudi zao leo nchini humo ambapo mrengo wa upinzani umeanza tena kutoa wito kwa umma kufanya maandamano ya kumshinikiza rais Ibrahim Boubcar Keita kuondoka afisini miaka mitatu kabla ya hatamu yake kukamilika.

Marais wengine wanne kutoka kanda ya Afrika ni pamoja na Macky Sall wa Senegal, Alassane Ouattara wa Ivory Coast, Mahamadou Issoufou wa Niger ambaye pia ni rais wa jumuiya ya ECOWAS na Nana Akufo-Addo wa Ghana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *