Boti ya wavuvi yazama malindi

Wavuvi chini ya usimamizi wa shughuli za bahari eneo la  Malindi kaunti ya Kilifi, wanaitafuta mashua moja iliyoripotiwa kuzama maji katika eneo la Mambrui jana jioni.

Mwenyekiti wa  usimamizi wa ufuo wa bahari eneo la Shella Aboud Sahe BMU, amesema kuwa mashua hiyo ilikuwa imetoka kaunti ya Lamu kuelekea mjini Malindi ilipopatwa na mkasa huo.

Kulingana na Sahe, huenda kifaa hicho kilikumbwa na hitilafu za kimitambo kabla yakuzama.

Hata hivyo, mwenyekiti huyo amebainisha kuwa vijana waliokuwa kwenye mashua hiyo waliokolewa na kwamba wako salama.

Huku hayo yakijiri, Sahe amezidi kuwahimiza wavuvi wa eneo hilo kuwa waangalifu zaidi wakati huu kunaposhuhudiwa mawimbi makali baharini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *