KEBs yapiga marufuku kampuni tatu kwa kutengeneza barakoa duni

Shirika la ukadriaji ubora wa bidhaa humu nchini (KEBs), limezipiga marufuku kampuni tatu za kutengeneza barakoa kwa kujihusisha na utengenezaji wa barakoa duni.

Taarifa iliyotolewa ilisema shirika hilo limefanya uchunguzi kote nchini kuhusu barakoa na kubaini kuwa baadhi ya watengenezaji bidhaa walagai wanajinufaisha na hali iliyoko sasa na kuuza vifaa duni.

Barakoa hizo ni pamoja na zile za WAMNDAS kutoka kampuni ya Wandas General Supplies, ARAX kutoka Arax Mills na pia zile za kampuni ya Hela Intimates EPZ.

Taarifa ya shirika hilo ilisema utumizi wa barakoa duni ama utumizi usiofaa ni hatari zaidi kwani unawapa Wananchi dhana potovu kwamba wamejikinga na hivyo kuongeza hatari ya kuambukizwa virusi vya Corona.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *