Aubameyang Kumwaga Wino Wa Miaka Mitatu Ndani Ya Arsenal

Mshambuliaji wa Arsenal na Gabon Pierre-Emerick Aubameyang atasaini mkataba mpya wa miaka mitatu na klabu hiyo utakaomfanya kuwa mchezaji anayelipwa zaidi klabuni hapo.

Mshambuliaji wa Tanzania, Mbwana Samatta ataweza kuondoka Aston Villa miezi minane tu baada ya kujiunga na klabu hiyo.

Kwengineko ni kuwa Chelsea imekataa ofa ya Inter Milan kwa ajili ya kiungo wake aliyetwaa kombe la dunia N’Golo Kante, ofa ambayo inajumuisha kubadilishana na kiungo wa Croatia Marcelo Brozovic.

Mlinzi wa Manchester United Muingereza Chris Smalling mwenye umri wa miaka 30 hajahudhuria mazoezi wiki hii akikaribia kutua ligi ya Italia, Serie A, kwenye timu ya Roma, kwa uhamisho wa kudumu, timu ambayo aliichezea kwa mkopo msimu uliopita.

Ndani ya Anfield nikuwa kiungo Georginio Wijnaldum mwenye miaka 29 amefanya mazungumzo yaliyoenda vizuri na meneja Jurgen Klopp kuhusu mustakabali wake klabuni hapo.

Mholanzi huyo amebakiza mwaka mmoja kwenye kandarasi yake ya sasa pale Anfield.

Beki wa England na Tottenham Rose anakaribia kutimka ligi kuu ya Uingereza kujiunga na kikosi cha Serie A Genoa.

Kipa wa Arsenal Muargentina Emiliano Martinez  amekubali kandarasi ya miaka mine na Aston Villa, yenye thamani ya pauni 60,000 kwa wiki, wakati huo vilabu hivyo vikitarajiwa kukubaliana ada ya uhamisho ya zaidi ya pauni milioni 15.

Kiungo wa Manchester United na Brazil Fredamepuuza ripoti kwamba anaweza kuondoka msimu huu na kujiunga Galatasaray na Uturuki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *