Aliyekua Mbunge wa Changamwe Kajembe ameaga dunia

Aliyekua Mbunge wa Changamwe Ramadhan Seif Kajembe ameaga dunia.

Kajembe ameaga katika Hospitali ya Pandya mjini Mombasa.

Itakumbukwa kuwa ni wiki mbili tu baada ya mkewe wa pili kufariki kwa kile kilichosemekana kuwa na maambukizi ya virusi vya Corona.

Gavana wa kaunti ya Mombasa Hassan Ali Joho ni mmoja wa viongozi wakuu kutoka ukanda wa pwani waliotoa rambirambi zao kwa familia ya marehemu Kajembe akisema eneo la pwani na Kenya nzima kwa jumla imepoteza kiongozi shupavu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *