Afisi ya DPP kutoa ratiba ya mpangilio wa jinsi kesi zitakapo-wasilishwa kupitia njia ya mtandao

Afisi ya Mkurugenzi Mkuu wa Mashtaka ya Umma leo inatarajiwa kutoa ratiba ya mpangilio wa jinsi kesi zitakapo-wasilishwa kupitia njia ya mtandao.

Kulingana na Mkurugenzi mkuu wa mashtaka ya umma Noordin Haji, ratiba hiyo mpya inanuiwa kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora.

Kupitia mtandao wake wa twitter, mkurugenzi huyo amesema kwamba jinsi ya kushughulikia kwa kesi mahakamani ni lazima ibadilishwe.

Mpangilio huo mpya itazingatia jinsi habari itakavyo-wasilishwa na kesi zitakapo-shughulikiwa. Hatua hiyo pia itahakikisha kuwepo kwa uwazi na kuhakikisha afisi hiyo inawajibika .

Pia imechukua uamuzi wa kuwakilisha mashataka bila upendeleo wowote.

Haji amesema amechukua jukumu la kuhakikisha kwamba kuna mabadiliko ili kuhakikisha wananchi wanashughulikiwa na kuafikia viwango vya kimataifa.

Aliongeza kwamba afisi yake itashirikiana na washirika wote kuhakikisha kuna huduma bora.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *