Acheni kuwagonganisha wakenya,Ruto awaonya wanasiasa.

Naibu rais Dr. William Ruto ametoa wito kwa wanasiasa kusita kuwagonganisha waKenya kwa manufaa yao binafsi kisisitiza kuwa ghasia hazipaswi kuruhusiwa kamwe kupenyeza katika siasa za taifa hili.

Akiongea nyumbani kwake huko Karen wakati wa hafla ya maombi iliyohudhuriwa na viongozi wa kidini na kisiasa kutoka kaunti ya Narok,naibu rais alisema kuwa wakenya wanataka viongozi wenye ajenda ya maendeleo kwa taifa hili.

Aliongeza kwamba wanaonufaika na migawanyiko,chuki na ghasia za kisiasa watapigwa na butwaa kwa vile wakenya wanataka umoja huku akiwahakikishia wakenya kwamba serikali haitaruhusu wanaoeneza siasa duni kufaulu.

Naibu wa rais vile vile alisema serikali itahakikisha kwamba mfumo wa ugavi wa mapato unawanufaisha wakenya wote kwani ilichaguliwa kuwahudumia wakenya wote bila kuwabagua.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *