Achani ahimiza serikali kuongeza Mgao wa fedha kwa kaunti

Naibu gavana wa kaunti ya Kwale Fatuma Achani ameitaka serikali ya kitaifa kuongeza mgao wa fedha kwa serikali za kaunti ili kuhakikisha kwamba wakaazi wa mashinani wanafaidika na maendeleo.

Akizungumza katika eneo bunge la Matuga, Achani amesema kuwa nyongeza ya mgao huo utazisaidia pakubwa kaunti zilizosalia nyuma kimaendeleo.

Akitoa mfano wa maendeleo hayo, Achani ameeleza jinsi kaunti ya Kwale imeanzisha mradi wa uchimbaji wa mabwawa katika maeneo kame. 

Aidha amedokeza kuwa mradi huo unalenga kupiga jeki sekta ya kilimo hasa katika maeneo hayo yanayokumbwa na tatizo la maji.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *